Friday 24 June 2011

NGOMEZI

MIVIGHA
Miviga (mivigha) ni sherehe zinazofanywa  na jamii katika kipindi maalumu cha mwaka zikiandamana na kanuni na matendo fulani. Sherehe hizi hufanywa katika kipindi maalum, huwa na sababu maalum na hufuata utaratibu maalum kwa kuzingatia viviga fulani maalum. Aghalabu kippindi hicho huwa baada ya mavuno katika jamii nyingi. Hii ni kwa sababu hakuna pilikapilika nyingi, bali wanajamii huwa katika hali ya furaha, buraha na mapumziko.
Mivigha hufanywa na jamii kwa lengo la kufundisha jambo ama msingi fulani maalumu kwa maisha ya vijana wao. Mivigha hufanyiwa mtu aliye katika hatua ya kuvuka kutaka kidato kimoja hadi kingine kama kutoka utoto hadi utu uzima. Vijana hufanyiwa mivigha baada ya kubaleghe (wavulana), au kuvunja ungo (wasichana). Wasichana wasiopitia mivigha huitwa wasungo ili kuwakebehi.
Mivigha hufundisha mambo kadha
(a)    Umuhimu wa kazi kama kilimo, uwindaji, uhunzi, ushonaji, ufinyanzi, uvuvi
(b)   Umuhimu wa ujasiri na nafasi yake katika suala zima la ulinzi kwa familia na jamii
(c)    Unyumba na malezi kwa jumla kama vile uzazi na malezi bora
Baada ya mafunzo hayo vijana wanaohusika hutahiriwa.  Mivigha ya kuwatahiri wavulana huitwa jando ilhali ile ya wasichana ni unyago. Wanaohusika kuwafunza vijana hawa ni watu wazima wanaozijua ada zote za jamii na mbinu muhimu za kuwafundisha vijana hawa. Walimu hawa huitwa kungwi kwa wanawake na ngariba kwa wanaume. Kazi ya kuwafundisha vijana hawa huitwa kufunda.
Shughuli za mivigha hufanywa mbali na nyumba za watu kama vile maporini, milimani, mtoni, pangoni, au chini ya mti maalumu “hekalu”. Ni nadra mivigha kufanyiwa karibu na nyumbani

Mvigha
Shughuli
Jando
Kutahiri wavulana
Unyago
Kutahiri wasichana
Akika
Kumnyoa mtoto
Harusi
Ndoa

Talaka
Tambiko
Kutambika

Kupatanisha wanajamii
Sihiri, uganga
Kuandua msiba

Kutoa shukrani za mavuno

Sherehe za kuanza ujenzi
Mazishi/ matanga
Kifo
Sifa
(a)    Hufanyiwa mahali maalumu
(b)   Huwa na msingi wa matukio fulani katika jamii husika
(c)    Huenda na wakati au majira maalum
(d)   Huongozwa na watu maalum (kungwi/ ngariba). Wanajamii wengine hufuata matukio tu
Umuhimu
(a)    Nyenzo ya kupitisha mawazo muhimu kuhusu jamii
(b)   Mojawapo ya vitambulishi vya jamii husika
(c)    Kufundisha wanajamii umuhimu wa kujitambulisha na jamii yao
(d)   Kufundisha mambo muhimu maishani  kama vile kutoa shukrani, utu uzima, ujasiri
(e)   Kuendeleza elimu ya jadi katika jamii
(f)     Kukabiliana na hali kama kifo au msiba fulani
(g)    Kielelezo chema kuendeleza ushirikiano wa wanajamii
(h)   Kukuza umoja na utangamano wa wanajamii
(i)     Kuikuza imani ya jamii husika
(j)     Kuendeleza elimu na utamaduni wa jamii
Hasara za Mivigha
(a)    Kuendeleza desturi zilizopitwa na wakati kama ukeketaji wa wasichana. Unyago ni sherehe unayomdhalilisha mtoto msichana na kumnyima haki ya kusoma
(b)   Baadhi ya mivigha hukuza matendo yaendayo kinyume na malengo ya kitaifa na mazingira. Kuwaaa wanyama fulani ni mfano ili kupewa cheo katika jamii ni mvigha yenye hasara
(c)    Huweza kuwa msingi wa utengano kati ya matabaka fulani katika jamii au makabila
(d)   Baadhi huweza kusambaza hofu miongoni mwa wanajamii hasa mivigha inayohusu viapo vya ulipaji kisasi
(e)   Huchangia kueneza magonjwa harari kama Ukimwi ambapo vijana hutahiriwa wakitumia kisu kimoja

No comments:

Post a Comment