Tasinifu hii inatalii matumizi ya nadharia ya vitendo usemi
katika kusuluhisha matatizo ya tafsiri ya Kiswahili. Msisitizo umatiliwa kwenye
ngazi ya ilokusheni ambapo swali kuu linaloongooza utafiti wenyewe ni kwamba
kutatokea nini iwapo tutahuruji nadharia ya VU na kuzitumia kama msingi wa
kushughulikia tatizo la tafsiri ya Kiswahili? Msimamo wetu ni kwamba nadharia
ya vitendo usemi inaweza kuwa faafu, lakini iwapo, mihimili yake itaeleweka na
jinsi VU huibuliwa katika LL. Miundo ya kuibua VU ambavyo tumeainisha kwa
kuzingatia kielelezo cha Searle imeshughulikiwa. Lengo letu ni kutambua kiwango
ambacho kwacho nadharia hii inaweza
kusuluhisha tatizo la ulinganifu wa maana katika tafsiri.
Tasnifu itajengwa kwenye sura sita. Sura
ya kwanza ni utangulizi unaofafanua suala la utafiti, madhumuni, ufafanuzi wa
nadharia na njia za utafiti. Katika sura ya pili tunaeleza dhana mbalimbali
ambazo zinahusu mada yetu ya utafiti kama vile nadharia ya VU pamoja na maswala
ya kimsingi kuhusu nadharia ya tafsiri, ili kuijengea mada yetu mihimili
thabiti ya kinadharia. Sura ya tatu, ya nne na ya tano ndizo kiini cha utafiti
wetu ambazo zitahusu uchanganuzi na uchambuzi
wa VU mahususi kutoka vitabu tulivyoviteua. Katika sura ya tatu tunashughulikia
VU na tafsiri kwa mkabala wa kimapokeo. Katika Sura ya nne tunashughulikia VU
katika vitabu hivyo hivyo kwa kuzingatia lugha ya kifasihi. Sura ya tano tunajihusisha
na VU kwa kuzingatia lugha ya ishara inayojitokeza katika vitabu hivyo hivyo.
Kwenye sura ya sita tunashughulikia uchambuzi na uchanganuzi wa matokeo ya
uchunguzi wetu na athari zake, yanayojitokeza kuhusu nadhariatete, ufaafu wa
mwongozo wetu wa utafiti na hatimaye mapendekezo.
Istilahi muhimu: vitendo usemi, lokusheni, ilokusheni, palokusheni, Searle, tafsiri
No comments:
Post a Comment